Wednesday, August 22, 2012

MISS TANZANIA 2012 AREJEA NYUMBANI KUTOKA MISS WORLD CHINA

 





Mrembo Lisa Jensen ambaye ni Miss World Tanzania 2012 amerejea jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini China alipokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia mwaka huu na kupokelewa na viongozi kadhaa wa Kamati ya Miss Tanzania akiwepo Mkurugenzi wa Kino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania Hashim Lundenga (kulia) aliyefika uwanja wa ndege wa JNIA Dar es salaam kumpokea.
Lisa akizungumza na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, kutoka kushoto, Katibu Mkuu, Bosco Majaliwa, Mrembo Amisa Hassan, Mkurugenzi Hashim Lundenga na Ofisa Habari wa Kamati, Haidan Rico
Lisa akila pozi ya picha na mmoja wa warembo waliofika kumpokea Amisa Hassan. Lisa alifanikiwa kuingia Robo fainali za Top Model na kumi bora ya Shindano la Multmedia Award

''Kaa kando'' Todd Akins aambiwa

 

Mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican , Mitt Romney, amemtaka mwanasiasa mwenzake wa chama hicho kujiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa kiti cha Useneta baada ya kutoa matamshi yaliyozua utata kuhusu ubakaji.

Mwanasiasa wa bunge la Congress, Todd Akin
Todd Akin, ambaye ni mwanasiasa wa bunge la Congress alizua manung'uniko kwa kudai kuwa mwili wa mwanamke una uwezo wa kuzuia mimba katika baadhi ya matukio ya ubakaji.
Matamshi ya Todd Kin anayegombea kiti cha seneta nchini Marekani yalitolewa wakati wa mahojiano. Alikuwa akitetea msimamo wake dhidi ya utoaji mimba.
Alipoulizwa kuhusu kutoa mimba iwapo mwanamke atabakwa, Todd Kin alieleza kuwa katika ubakaji halali au kile alichokitaja kuwa 'legitimate rape' kuna uwezekano kwamba kibiolioia, mwili wa mwanamke utamzuia kupata mimba anapobakwa.
Matamshi yake yamezua hisia kali.
Mpinzani wake Mitt Romney amesema, ''Matamshi yake kuhusu ubakaji yanaudhi sana na siwezi nikatetea msimao wake au nikamtetea yeye''
Baadhi ya wenzake Todd Akin kutoka chama cha Republican wamemtaka kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha useneta.
Hiki ni kipindi kigumu kwa wana Republican ambao walikuwa wamejiandaa kuendeleza kampeni yao kwa kumshambulia rais Obama kwa jinsi uchumi ulivyozorota wakati wa uongozi wake. Badala yake sasa wamejikuta wakirushiana maneno kuhusu sera za kijamii.
Chama cha Democrats kimechukua fursa hiyo kushambulia Republicans kwa kuwataja kama watu ambao hawazingatii maslahi na hisia za wanawake.
Todd Akin ameomba msamaha kufuatia matamshi yake.
"Nilitumia maneno yasiofaa na ninaomba msamaha. Nina watoto wawili wa kike na nataka haki kutendeka, nina roho ya huruma kwa waathiriwa wa ubakaji na nawaombea. Ukweli ni kuwa, mtu anaweza akapata mimba kutokana na ubakaji. Ukweli ni kwamba, kuna waathiriwa wengi wa ubakaji. Makosa yangu ni kutumia maneno yasiofaa. Naomba msamaha wako. ''
Hata hivyo halitakuwa jambo la kushangaza iwapo atalazimika kujiondoa kwenye mbio za kuwania kiti cha useneta kwa sababu ya matamshi hayo.

Rais wa Liberia amsimamisha kazi mwanae

Ellen Johnson Sirleaf anashutumiwa kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu
Ellen Johnson Sirleaf anashutumiwa kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, amemsimamisha kazi mmoja wa watoto wake wa kiume kutoka ngazi ya unaibu gavana wa benki kuu ya nchi hiyo kwa kushindwa kuorodhesha mali zake katika tume ya kuzuia rushwa nchini humo.
Charles Sirleaf, ni miongoni mwa maafisa 46 waliosimamishwa kazi kwa kosa hilo.
Ni mmoja wa watoto wake watatu wa kiume aliowateua kushika vyeo vya juu kabisa baada ya kushinda muhula wa pili wa uchaguzi mwaka jana.
Wapinzani wa Bi Sirleaf wanamshutumu kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu.
Rais huyo amemteua mtoto wake wa kiume Fumba kuwa mkuu idara ya usalama wa taifa, na kijana mwingine Robert kuwa mshauri mkuu na mwenyekiti wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali-NOCAL.

Utawala bora

Robert Sirleaf anayashitaki magazeti mawili nchini humo ya Independent na Analyst, na mwanasiasa wa upinzani Jefferson Kogie kwa kumkashifu kuwa amejinufaisha kifedha kutokana na vyeo alivyopewa.
Taarifa kutoka ofisi ya Bi Sirleaf imesema Charles Sirleaf na maafisa wengine 45 wataendelea kuwa wamesimamishwa kazi hadi hapo watakapoorodhesha mali zao kwa Tume ya Kuzuia Rushwa.
Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na mkuu wa itifaki ya rais, David Anderson, Wakili mkuu na naibu waziri wa sheria Micah Wilkins Wright na naibu mkurugenzi mkuu wa utangazaji Ledgerhood Rennie.
Liberia
Liberia

Bi Sirleaf aliyeingia madarakani mwaka 2005 mwishoni mwa mgogoro wa vita Uliodumu miaka 14, amekuwa akiahidi mara kwa mara kupambana na rushwa na kustawisha utawala bora nchini Liberia.
Alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka jana, muda mfupi baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine katika uchaguzi ulioghubikwa na tuhuma za udanganyifu katika zoezi la upigaji kura.
Rushwa bado inabakia kuwa kikwazo kikubwa nchini Liberia huku idadi kubwa ya watu wakiishi katika umasikini licha ya utajiri mkubwa wa madini nchini humo.
Mwezi Juni taasisi ya kimataifa ya Maafa-ICG, ilitoa ripoti kutahadharisha kuwa rushwa na upendeleo wa kindugu katika sekta mbalimbali vinaweza kuhatarisha demokrasia nchini humo.

Tuesday, July 31, 2012

MGOMO WA WALIMU IRINGA WASHINDIKANA



Mwanafunzi wa darasa la Herieth Kitunduru akiwakumbusha masomo wanafunzi wa darasa la tano leo baada ya walimu kugoma
Mkuu wa shule ya Mtwivila Christabela Alfani ambaye ametelekezewa shule ya walimu wenzake leo
Wanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Kihesa wakiendelea kufundishwa leo baada ya walimu wao kugomea mgomo wa walimu
Mkuu wa shule ya msingi Kihesa Zabihu Hassan akiwa kazini
Mwalimu wa shule ya Msingi Kihesa akiendelea na kazi leo
hivi ndivyo walivyofanya walimu wa Mtwivila Iringa kwa kujiorodhesha bila kuwepo kazini
                                          Wanafunzi wa darasa la tano
Mkuu wa shule ya Msingi Wilolesi Gabriel Kameka akiendelea na kazi kama kawaida

Mmarekani akiri njama kusaidia al-Shabab


Wapiganaji wa al-Shabab
Mmarekani aliyetuhumiwa kwa kujaribu kujiunga na kundi lenye msimamo mkali la Kiislam la al-Shabab nchini Somalia amekiri mashtaka yake kwenye mahakama Marekani.
Shaker Masri, 28, alikamatwa Agosti 2010 akijiandaa kusafiri kwenda Somalia kukijunga na al-Shabab, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Marekani.
Marekani na Uingereza wanaliona kundi hilo likijihusisha na al-Qaeda, kuwa ni kundi la kigaidi.
Katika makubaliano ya kukubali mashtaka, Masri amekubali kutumikia kifungo chini ya miaka kumi gerezani.
Alikiri kupanga njama za kukusanya fedha alizohitaji kujzitumia katika jihadi ama Somalia au Afghanistan.
Amehukumiwa kifungo za miaka 15 gerezani.
Masri alizaliwa Alabama na kuishi Chicago kabla ya kukamatwa saa chache hajaondoka nchini.
Amekuwa akijieleza kama wakala wa FBI wa siri na amekuwa akizungumzia kuhusu kuwalenga ‘makafiri’
Kufuatia kukamatwa kwake alishtakiwa kwa kujaribu kusaidia kwa mali kundi la kigaidi, akijaribu kuwapa msaada kwa kutumia silaha za maangamizi.
Taarifa kamili za kukiri kwake hazijatolewa kwa umma.
Al-Shabab wanaamini kuwa ikiwapata wasomali wenye asili ya Kimarekani kushiriki katika kujitoa muhanga nchini Somalia na maafisa wa Marekani sasa wana wasiwasi wa kuwepo shambulio ndani ya Marekani.
Raia kadhaa wa Marekani wamekamatwa katika miaka ya karibuni wakijaribu kushiriki au kuunga mkono vita vya zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Shaker Masri atahukumiwa rasmi mwezi Oktoba 16.

Biashara ya dawa haramu yazidi G. Bissau

Wanajeshi wa Guinea Bissau, UN yaonya juu ya dawa za kulevya
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonyesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa biashara ya dawa za kulevya Guinea-Bissau tangu mapinduzi yatokee mwezi April.
Limetaka viongozi nchini humo kurejesha utawaa wa kikatiba.
 
Guinea-Bissau imekuwa na hisotria ya mapinduzi tangu uhuru wake kutoka kwa Mreno mwaka 1974.
Imekuwa ndio kitovu cha magenge ya kupitishia cocaine kutoka Latin America mpaka Ulaya, ikituhumiwa kushirikiana na maafisa wa jeshi.
"Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani kitendo cha jeshi kuingilia siasa na kuonyesha wasiwasi wake kuhusu taarifa za kuongezeka kwa usafirishaji wa dawa kuongezeka tangu April 12 mapinduzi yalipotokea." Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilisema katika mkutano wake New York.
Limesema lilikuwa linaangalia uwezekano wa mkutano wa kimataifa kuzungumzia ni kwa namna gani watafanikiwa kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini Guinea Bissau.
'Ushawishi'
Mwezi Mei , Baraza hilo liliweka vikwazo vya kusafiri kwa viongozi wa mapinduzi na wanaowaunga mkono.
Jeshi limekubali mazungumzo yasimamiwe na ECOWAS, kurejesha nchi katika utawala wa demokrasia lakini limeshindwa kufanya hivyo.
Mwaka 2010, Marekani iliwashutumu wanajeshi kutoka Guinea-Bissau, wakiwemo mkuu wa jeshi la majini Jose Americo Bubo Na Tchuto, kwa kuhusika na dawa za kulevya.
Katika sheria ya Ushawishi wa Dawa za kulevya , vikwazo vya kifedha viliwekwa.
Hakuna wa kuchaguliwa kwa karibu miaka arobaini sasa ya uhuru ambaye amewahi kumaliza muda wake wa uongozi nchini Guinea-Bissau.

Mwanamke Vietnam ajichoma moto

 
Mwanamke mmoja wa Ki-Vietnam anaripotiwa kufa kwa majeraha ya moto baada ya kujichoma mwenyewe mbele ya ofisi ya serikali ya mtaa.
Ndugu mmoja wa familia amesema alikuwa anapinga kitendo cha binti yake kuzuiliwa kwa tuhuma za kupinga propaganda za nchi.
Amesema alikufa akiwa anapelekwa hospitali mjini Ho Chi Minh.
Binti wa mwanamke huyo Ta Phong Tan, alikuwa polisi na mwana blogu ambaye alizuiliwa mwaka jana baada ya kuonyesha vitendo vya kikatili na unyanyasaji vinavyofanywa na polisi.

BAADHI YA WAMILIKI WA BLOG ZA KIJAMII WAKIWA WAMESHIKILIA TUZO ZAKO

MASOUD KIPANYA AKIWA AMESHIKA TUZO NA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA VODACOM.

MTANGAZAJI NA DJ WA CLOUDS FM AKIFURAHI BAADA YA KUTUNUKIWA TUZO

AMA KWELI MAISHA MUNGU MWENYEWE NDIO ANAJUA,KANUMBA PUMZIKA KWA AMANI SISI TUPO TUNAKUOMBEA NAAMINI KILA MOJA ATAYAONJA MAUTI



Ni majonzi makubwa sana kwa Watanzania wote sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi, inauma sana kwa kijana mdogo kama Kanumba kufariki wakati alikuwa bado hajazitima ndoto zake .Mungu ailaze roho ya marehemu Swaiba wangu Steven Kanumba ni mengi sana tuliyoyafanya mimi na wewe katika gurudumu ili la sanaa bila kujali yote yaliyotokea ni kawaida ya binadamu kutoelewana kama Baba na Mama wanafunga ndoa kanisani na wanakula viapo vya utii mbele za Mungu lakini wanagombana na kufikia hatua ya kuachana kwanini ishindikane kwetu ni hali ya kwaida katika maisha binadamu kutofautiana mengi yanazungumzwa juu yangu ila kila kitu mimi namuachia Mungu mimi ni mnyonge siwezi kupambana nanyi mnaoniongelea vibaya maumivu nayoyapata juu yenu Mungu hatowaacha siwezi kuzizuia hisia zenu kuzungumza yale mnayojisikia.

Muda mfupi tu baada ya kufariki Steven Kanumba akiwa kwenye gari lake la kifahari Lexus tangulia ndugu yangu sisi tuko nyuma yako maana kila nafsi itaonja umauti. Wadau nilikuwa kimya kwa kutowaletea matukio kwa sababu ya shughuli zilkuwa nyingi sana katika msiba nilikuwa kwenye kamati ya mazishi hivyo sikuwa nikipata muda wa kutosha na sio watu wanavyofikiria jamani hata kama kuna matatizo ndio katika maswala ya msiba hapana jamani mimi sijafikia hali hiyo yakuwa na roho ya kinyama namna hiyo

Hapa tukiutelemsha mwili wa marehemu katika hospital ya Muhimbili ni mtu wa kwanza kufika katika eneo la tukio

Tukimfunika rafiki yetu katika safari yakuelekea mochwali

Safari yetu ya mwisho binadamu wote mara ya kwanza nilipofika walikataa kumpokea pale hospital mpaka wapate PF 3 ndipo nilipowasha gari na kwenda Salenda polisi na kuwapata askari watatu ndipo tukapata fursa ya kwenda kumpuzisha marehemu

Tukimfunika macho maana yalikuwa wazi kama anasinzia

Macho yakiwa yamefumba baada ya kumfumba

RAY AINGIZA THE GLORY OF RAMADHAN

 
 


Kazi ikifanyika.

Vijana wakiwa makini na script kabla ya scene kuanza kushutiwa
Batuli(Neshi).

Mmmmmmmm ni hatari sana futari drafti

On Set

Hii ni moja ya filamu bora ya dini ambayo itatikisa sana sokoni.

On set

Tukiendelea na kazi

Monday, July 30, 2012

MKE WA WAZIRI MKUU TUNU PIUNDA AZINDUA MRADI WA MAJI HOSPITAL YA MAWENZI KILIMAJARO


Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifunua pazia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi mjini Moshi, mradi huo ambao umefadhiliwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL umegharimu zaidi ya milioni 55 za kitanzania ulilenga kutoa suluhisho la muda mrefu katika matatizo sugu yayoikumba jamii hususani tatizo la uhaba wa maji safi kwa maendeleo ya maisha ya mtanzania, Kushoto katika picha ni Mkuu wa Wialaya ya Moshi Dk Msengi na yana uwezo wa kuhifadhi lita elfu 40.000 kwa wakati mmoja
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti B. Teddy Mapunda akitoa maelezo ya mradi huo kwa mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Bw. Richard. Wells anayemaliza muda wake.
Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon akifungua bomba la maji mara baada ya mama Tunu Pinda anayeshuhudia tukio hilo kuzindua mradi huo kwenye hospitali ya Mkoa ya Mawenzi mjini Moshi leo, wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk Msengi na kushoto ni Mkurugenzi wa Serengeti SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells.
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akizungumza katika uzinduzi huo huku wakuu wa kampuni ya bia ya Serengeti wakimsikiliza kutoka kushoto ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa SBL Bw. Steve Gannon na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake Richard Wells.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo huku mgeni rasmiMama Tunu Pinda akifuatilia kwa makini.
Kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na uwajibikaji Bw. Malisa, Imani Lwinga Meneja Mawasiliano na Mtaalamu Masuala ya Fedha SBL Bw. John Collins.
Haya ndiyo Matenki ya maji katika mradi huo yataweza kuhifadhi lita elfu 40.000 za maji.
Mmama Tunu Pinda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya kuzindua mradi wa maji kutoka kulia ni Mkurugenzi mpya wa SBL Bw. Steve Gannon, Mkurugenzi wa SBL anayemaliza muda wake B. Richard Wells na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells mara baada ya kuwasili kwenye Hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa maji, kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL na Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo Bw. Steve Gannon.
Kutoka kulia ni Mganga mkuu wa Mkoa wa Kiliamjaro Dk Mtumwa Mwako Steve Gannon, Richard Wells na Teddy Mapuinda wakimsubiri mgeni rasmi.

Mgeni rasmi mama Tunu Pinda akiwasili katika eneo la Tukio.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Ephraim Mafuru.
Baadhi ya wauguzi na wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Teddy Mapunda akizungumza katika uzinduzi huo.
Bw. Richard Wells naye akatoa neno.
Wakuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti mstari wa mbele ni kutoka kulia ni Mkurugenzi mpya wa Kampuni ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon na Teddy Mapunda mstari wa nyuma kutoka kulia John Collins Mtaalam wa Fedha, Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji na Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko.
Mama Tunu Pinda akimsikiliza Bw. Richard WellsMkurugenzi wa SBL wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika hospitali ya Mawenzi leo.
Mkurugenzi wa Masoko SBL Bw. Ephraim Mafuru akizungumza katika mkutano huo.
Mama Tunu Pinda akipanda mti katika hospitali ya Mawenzi mara baada ya kuzindua mradi wa maji hospitalini hapo