WWW.JOSHUA.BLOGSPOT.COM

Tuesday, July 31, 2012

MGOMO WA WALIMU IRINGA WASHINDIKANA



Mwanafunzi wa darasa la Herieth Kitunduru akiwakumbusha masomo wanafunzi wa darasa la tano leo baada ya walimu kugoma
Mkuu wa shule ya Mtwivila Christabela Alfani ambaye ametelekezewa shule ya walimu wenzake leo
Wanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Kihesa wakiendelea kufundishwa leo baada ya walimu wao kugomea mgomo wa walimu
Mkuu wa shule ya msingi Kihesa Zabihu Hassan akiwa kazini
Mwalimu wa shule ya Msingi Kihesa akiendelea na kazi leo
hivi ndivyo walivyofanya walimu wa Mtwivila Iringa kwa kujiorodhesha bila kuwepo kazini
                                          Wanafunzi wa darasa la tano
Mkuu wa shule ya Msingi Wilolesi Gabriel Kameka akiendelea na kazi kama kawaida
Posted by Unknown at 7:37 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Mmarekani akiri njama kusaidia al-Shabab


Wapiganaji wa al-Shabab
Mmarekani aliyetuhumiwa kwa kujaribu kujiunga na kundi lenye msimamo mkali la Kiislam la al-Shabab nchini Somalia amekiri mashtaka yake kwenye mahakama Marekani.
Shaker Masri, 28, alikamatwa Agosti 2010 akijiandaa kusafiri kwenda Somalia kukijunga na al-Shabab, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Marekani.

 

Marekani na Uingereza wanaliona kundi hilo likijihusisha na al-Qaeda, kuwa ni kundi la kigaidi.
Katika makubaliano ya kukubali mashtaka, Masri amekubali kutumikia kifungo chini ya miaka kumi gerezani.
Alikiri kupanga njama za kukusanya fedha alizohitaji kujzitumia katika jihadi ama Somalia au Afghanistan.
Amehukumiwa kifungo za miaka 15 gerezani.
Masri alizaliwa Alabama na kuishi Chicago kabla ya kukamatwa saa chache hajaondoka nchini.
Amekuwa akijieleza kama wakala wa FBI wa siri na amekuwa akizungumzia kuhusu kuwalenga ‘makafiri’
Kufuatia kukamatwa kwake alishtakiwa kwa kujaribu kusaidia kwa mali kundi la kigaidi, akijaribu kuwapa msaada kwa kutumia silaha za maangamizi.
Taarifa kamili za kukiri kwake hazijatolewa kwa umma.
Al-Shabab wanaamini kuwa ikiwapata wasomali wenye asili ya Kimarekani kushiriki katika kujitoa muhanga nchini Somalia na maafisa wa Marekani sasa wana wasiwasi wa kuwepo shambulio ndani ya Marekani.
Raia kadhaa wa Marekani wamekamatwa katika miaka ya karibuni wakijaribu kushiriki au kuunga mkono vita vya zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Shaker Masri atahukumiwa rasmi mwezi Oktoba 16.
Posted by Unknown at 7:30 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Biashara ya dawa haramu yazidi G. Bissau

Wanajeshi wa Guinea Bissau, UN yaonya juu ya dawa za kulevya
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonyesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa biashara ya dawa za kulevya Guinea-Bissau tangu mapinduzi yatokee mwezi April.
Limetaka viongozi nchini humo kurejesha utawaa wa kikatiba.
 
Guinea-Bissau imekuwa na hisotria ya mapinduzi tangu uhuru wake kutoka kwa Mreno mwaka 1974.
Imekuwa ndio kitovu cha magenge ya kupitishia cocaine kutoka Latin America mpaka Ulaya, ikituhumiwa kushirikiana na maafisa wa jeshi.
"Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani kitendo cha jeshi kuingilia siasa na kuonyesha wasiwasi wake kuhusu taarifa za kuongezeka kwa usafirishaji wa dawa kuongezeka tangu April 12 mapinduzi yalipotokea." Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilisema katika mkutano wake New York.
Limesema lilikuwa linaangalia uwezekano wa mkutano wa kimataifa kuzungumzia ni kwa namna gani watafanikiwa kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini Guinea Bissau.
'Ushawishi'
Mwezi Mei , Baraza hilo liliweka vikwazo vya kusafiri kwa viongozi wa mapinduzi na wanaowaunga mkono.
Jeshi limekubali mazungumzo yasimamiwe na ECOWAS, kurejesha nchi katika utawala wa demokrasia lakini limeshindwa kufanya hivyo.
Mwaka 2010, Marekani iliwashutumu wanajeshi kutoka Guinea-Bissau, wakiwemo mkuu wa jeshi la majini Jose Americo Bubo Na Tchuto, kwa kuhusika na dawa za kulevya.
Katika sheria ya Ushawishi wa Dawa za kulevya , vikwazo vya kifedha viliwekwa.
Hakuna wa kuchaguliwa kwa karibu miaka arobaini sasa ya uhuru ambaye amewahi kumaliza muda wake wa uongozi nchini Guinea-Bissau.
Posted by Unknown at 7:26 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Mwanamke Vietnam ajichoma moto

 
Mwanamke mmoja wa Ki-Vietnam anaripotiwa kufa kwa majeraha ya moto baada ya kujichoma mwenyewe mbele ya ofisi ya serikali ya mtaa.
Ndugu mmoja wa familia amesema alikuwa anapinga kitendo cha binti yake kuzuiliwa kwa tuhuma za kupinga propaganda za nchi.
Amesema alikufa akiwa anapelekwa hospitali mjini Ho Chi Minh.
Binti wa mwanamke huyo Ta Phong Tan, alikuwa polisi na mwana blogu ambaye alizuiliwa mwaka jana baada ya kuonyesha vitendo vya kikatili na unyanyasaji vinavyofanywa na polisi.
Posted by Unknown at 7:23 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

BAADHI YA WAMILIKI WA BLOG ZA KIJAMII WAKIWA WAMESHIKILIA TUZO ZAKO

MASOUD KIPANYA AKIWA AMESHIKA TUZO NA CHETI CHA UTAMBUZI KUTOKA VODACOM.

MTANGAZAJI NA DJ WA CLOUDS FM AKIFURAHI BAADA YA KUTUNUKIWA TUZO
Posted by Unknown at 7:11 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

AMA KWELI MAISHA MUNGU MWENYEWE NDIO ANAJUA,KANUMBA PUMZIKA KWA AMANI SISI TUPO TUNAKUOMBEA NAAMINI KILA MOJA ATAYAONJA MAUTI



Ni majonzi makubwa sana kwa Watanzania wote sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi, inauma sana kwa kijana mdogo kama Kanumba kufariki wakati alikuwa bado hajazitima ndoto zake .Mungu ailaze roho ya marehemu Swaiba wangu Steven Kanumba ni mengi sana tuliyoyafanya mimi na wewe katika gurudumu ili la sanaa bila kujali yote yaliyotokea ni kawaida ya binadamu kutoelewana kama Baba na Mama wanafunga ndoa kanisani na wanakula viapo vya utii mbele za Mungu lakini wanagombana na kufikia hatua ya kuachana kwanini ishindikane kwetu ni hali ya kwaida katika maisha binadamu kutofautiana mengi yanazungumzwa juu yangu ila kila kitu mimi namuachia Mungu mimi ni mnyonge siwezi kupambana nanyi mnaoniongelea vibaya maumivu nayoyapata juu yenu Mungu hatowaacha siwezi kuzizuia hisia zenu kuzungumza yale mnayojisikia.

Muda mfupi tu baada ya kufariki Steven Kanumba akiwa kwenye gari lake la kifahari Lexus tangulia ndugu yangu sisi tuko nyuma yako maana kila nafsi itaonja umauti. Wadau nilikuwa kimya kwa kutowaletea matukio kwa sababu ya shughuli zilkuwa nyingi sana katika msiba nilikuwa kwenye kamati ya mazishi hivyo sikuwa nikipata muda wa kutosha na sio watu wanavyofikiria jamani hata kama kuna matatizo ndio katika maswala ya msiba hapana jamani mimi sijafikia hali hiyo yakuwa na roho ya kinyama namna hiyo

Hapa tukiutelemsha mwili wa marehemu katika hospital ya Muhimbili ni mtu wa kwanza kufika katika eneo la tukio

Tukimfunika rafiki yetu katika safari yakuelekea mochwali

Safari yetu ya mwisho binadamu wote mara ya kwanza nilipofika walikataa kumpokea pale hospital mpaka wapate PF 3 ndipo nilipowasha gari na kwenda Salenda polisi na kuwapata askari watatu ndipo tukapata fursa ya kwenda kumpuzisha marehemu

Tukimfunika macho maana yalikuwa wazi kama anasinzia

Macho yakiwa yamefumba baada ya kumfumba
Posted by Unknown at 1:06 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

RAY AINGIZA THE GLORY OF RAMADHAN

 
 


Kazi ikifanyika.

Vijana wakiwa makini na script kabla ya scene kuanza kushutiwa
Batuli(Neshi).

Mmmmmmmm ni hatari sana futari drafti

On Set

Hii ni moja ya filamu bora ya dini ambayo itatikisa sana sokoni.

On set

Tukiendelea na kazi
Posted by Unknown at 12:57 AM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Monday, July 30, 2012

MKE WA WAZIRI MKUU TUNU PIUNDA AZINDUA MRADI WA MAJI HOSPITAL YA MAWENZI KILIMAJARO


,
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifunua pazia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi mjini Moshi, mradi huo ambao umefadhiliwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL umegharimu zaidi ya milioni 55 za kitanzania ulilenga kutoa suluhisho la muda mrefu katika matatizo sugu yayoikumba jamii hususani tatizo la uhaba wa maji safi kwa maendeleo ya maisha ya mtanzania, Kushoto katika picha ni Mkuu wa Wialaya ya Moshi Dk Msengi na yana uwezo wa kuhifadhi lita elfu 40.000 kwa wakati mmoja
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti B. Teddy Mapunda akitoa maelezo ya mradi huo kwa mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Bw. Richard. Wells anayemaliza muda wake.
Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon akifungua bomba la maji mara baada ya mama Tunu Pinda anayeshuhudia tukio hilo kuzindua mradi huo kwenye hospitali ya Mkoa ya Mawenzi mjini Moshi leo, wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk Msengi na kushoto ni Mkurugenzi wa Serengeti SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells.
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akizungumza katika uzinduzi huo huku wakuu wa kampuni ya bia ya Serengeti wakimsikiliza kutoka kushoto ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa SBL Bw. Steve Gannon na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake Richard Wells.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo huku mgeni rasmiMama Tunu Pinda akifuatilia kwa makini.
Kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na uwajibikaji Bw. Malisa, Imani Lwinga Meneja Mawasiliano na Mtaalamu Masuala ya Fedha SBL Bw. John Collins.
Haya ndiyo Matenki ya maji katika mradi huo yataweza kuhifadhi lita elfu 40.000 za maji.
Mmama Tunu Pinda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya kuzindua mradi wa maji kutoka kulia ni Mkurugenzi mpya wa SBL Bw. Steve Gannon, Mkurugenzi wa SBL anayemaliza muda wake B. Richard Wells na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa SBL anayemaliza muda wake Bw. Richard Wells mara baada ya kuwasili kwenye Hospitali ya Mawenzi kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa maji, kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL na Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo Bw. Steve Gannon.
Kutoka kulia ni Mganga mkuu wa Mkoa wa Kiliamjaro Dk Mtumwa Mwako Steve Gannon, Richard Wells na Teddy Mapuinda wakimsubiri mgeni rasmi.

Mgeni rasmi mama Tunu Pinda akiwasili katika eneo la Tukio.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Ephraim Mafuru.
Baadhi ya wauguzi na wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Teddy Mapunda akizungumza katika uzinduzi huo.
Bw. Richard Wells naye akatoa neno.
Wakuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti mstari wa mbele ni kutoka kulia ni Mkurugenzi mpya wa Kampuni ya Serengeti SBL Bw. Steve Gannon na Teddy Mapunda mstari wa nyuma kutoka kulia John Collins Mtaalam wa Fedha, Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji na Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko.
Mama Tunu Pinda akimsikiliza Bw. Richard WellsMkurugenzi wa SBL wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika hospitali ya Mawenzi leo.
Mkurugenzi wa Masoko SBL Bw. Ephraim Mafuru akizungumza katika mkutano huo.
Mama Tunu Pinda akipanda mti katika hospitali ya Mawenzi mara baada ya kuzindua mradi wa maji hospitalini hapo
Posted by Unknown at 11:17 PM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIMJUALIA HALI KIKONGWE KATIKA KIJIJI CHA MUSOGA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Bibi Antonia Mbagalla (85) katika kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze Wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki leo(Jumapili).(picha na Freddy Maro).
               KIKWETE AKIFURAHIA JAMBO NA KIKONGWE HUYO
  
Posted by Unknown at 10:33 PM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEMEJI YAKE MKOANI LINDI

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Julai 30, 2012 amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi (45), aliyefariki
Jumamosi iliyopita jijini Dar es salaam, na kuzikwa katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.
Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi leo Julai 30, 2012
PICHA NA IKULU
Posted by Unknown at 10:25 PM No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Newer Posts Older Posts Home
Subscribe to: Comments (Atom)

Blog Archive

  • ►  2013 (2)
    • ►  July (1)
    • ►  June (1)
  • ▼  2012 (44)
    • ►  August (3)
    • ▼  July (31)
      • MGOMO WA WALIMU IRINGA WASHINDIKANA
      • Mmarekani akiri njama kusaidia al-Shabab
      • Biashara ya dawa haramu yazidi G. Bissau
      • Mwanamke Vietnam ajichoma moto
      • BAADHI YA WAMILIKI WA BLOG ZA KIJAMII WAKIWA WAMES...
      • AMA KWELI MAISHA MUNGU MWENYEWE NDIO ANAJUA,KANUMB...
      • RAY AINGIZA THE GLORY OF RAMADHAN
      • MKE WA WAZIRI MKUU TUNU PIUNDA AZINDUA MRADI WA MA...
      • RAIS JAKAYA KIKWETE AKIMJUALIA HALI KIKONGWE KATIK...
      • RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEMEJI YAKE MKO...
      • Ebola Uganda ilianza kwa mja mzito
      • Mauaji ya balozi yachunguzwa Kenya
      • VIJANA WENGI WAJITOKEZA EBSS TANGA
      • DIWANI KATA YA KIVULE AKISAIDIA KUWAWEKA SAWA WATU...
      • DAH, HII PICHA NI BALAH
      • MSAMA AKISHIRIKIANA NA POLISI WAMEWAKAMATA WEZI WA...
      • Wahamiaji wasomali 90 wakwama baharini
      • Free Syrian Army wadhibiti Aleppo Imebadilis...
      • MLEMAVU wa viungo Isaya Keraryo Mkazi wa Bunda Sto...
      • TAASISI ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF),ime...
      • YANGA YAIFANYA VIBAYA APR,JAMANI WE ACHATU
      • Ugiriki yatamani misaada
      • Mwenge wa Olimpik washangiliwa Uingereza
      • Kim Jong-un amepata jiko
      • MELI YA MV SKAGT YAZAMA ZANZIBAR
      • MAAZIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA YALIVYOFANYA
      • MAONYESHO YA SABASABA YALIVYOFANA
      • BONGO MOVIE Vs BONGO FLAVA KATIKA USIKU WA TAMASHA...
      • WAPEMBA WALIOKIMBILIA SOMALIA NA KUOMBA HIFADHI W...
      • MHARIRI MKUU JAMBO LEO AFARIKI DUNIA
      • RAIS WA MADAKTARI AFIKISHWA MAHAKAMANI
    • ►  June (10)

About Me

Unknown
View my complete profile
Simple theme. Powered by Blogger.